MAMBO YA KUJIFUNZA KABLA HUJAWA MJASILIAMALI.
Jifunze mambo yafuatayo kabla ya kuwa mjasiliamali kwa jambo lolote ; (1): Learn how to sell ; Jifunze namna ya kuuza na kutangaza biashara yako.Pamoja na hayo utakutana na vipingamizi vingi ukianzisha biashara yako kwani watu wengine watakuponda,watakudharau na kukutukana lakini hapa utajifunza namna ya kujieleza wewe mwenyewe na kuiweka sehemu nzuri biashara yako. (2): Communication skills; Hapa ni kujifunza jinsi ya kuwasiliana na wateja au watu wanaokuzunguka unawasiliana nao kivipi, nikimaanisha; - Namna ya kukaa na watu. - Namna ya kutoa wazo lako kwa watu. - Kujifunza namna ya kuendesha biashara yako na uzoefu. (3): Customer services; Waamini na uwakubali wateja wako na uonyeshe nia...