MAMBO YA KUJIFUNZA KABLA HUJAWA MJASILIAMALI.

            Jifunze mambo yafuatayo kabla ya kuwa mjasiliamali kwa jambo lolote;


(1): Learn how to sell;
 Jifunze namna ya kuuza na kutangaza biashara yako.Pamoja na hayo utakutana na vipingamizi vingi ukianzisha biashara yako kwani watu wengine watakuponda,watakudharau na kukutukana lakini hapa utajifunza namna ya kujieleza wewe mwenyewe na kuiweka sehemu nzuri biashara yako.

(2): Communication skills;
Hapa ni kujifunza jinsi ya kuwasiliana na wateja au watu wanaokuzunguka unawasiliana nao kivipi, nikimaanisha;
       - Namna ya kukaa na watu.
       - Namna ya kutoa wazo lako kwa  
         watu.
       -Kujifunza namna ya kuendesha
           biashara yako na uzoefu.

(3): Customer services;
Waamini na uwakubali wateja wako na uonyeshe nia ya kuwahudumia na kuweza kujali huduma yako.

(4): Time management;
Thamini mda wa biashara yako na uutunze kwa kufuata ratiba.
Tumia mda wako vizuri, kwani biashara haileti faida kwa kuangalia mda ulioutumia kufanya biashara bali uthamani wa kitu ulichokifanya kwenye huo mda.
      ``time is money"

(5): Financial management;
Jifunze kutunza na kutumia fedha unayoipata na usiruhusu fedha ikuongoze wewe bali uiongoze wewe.
Usikubali fedha ikutawale.

(6):Networking;
Jifunze kuongeza mtandao wako katika mafanikio yako, kuwa na marafiki wenye mtizamo chanya,kuongea na watu,na usitake ufanikiwe wewe peke yako.

Comments

Popular posts from this blog

STRUGGLE MAKE YOU STRONGER.

UTAFANYA VITU GANI ILI KUFANIKISHA BIASHARA YAKO NA MAISHA KIUJUMLA