UTAFANYA VITU GANI ILI KUFANIKISHA BIASHARA YAKO NA MAISHA KIUJUMLA
Vitu vifuatavyo vinakusaidia kuanzisha shughuli yoyote au kukuongezea kipato katika maisha yako na kuonekana wa thamani;
1. Fanya kile kilicho ndani ya uwezo wako kutatua matatizo yako na kujiletea maendeleo,tafuta msaada pale juhudi zako zinapoishia.
2. Tambua vipaji na ujuzi ulionao na uweze kuvitumia ili zikuletee maendeleo.
3. Tumia fursa zilizopo karibu nawe kuanza na kujiendeleza.
4. Jiweke karibu na watu wenye mtizamo chanya,malengo na bidii .
5. Jenga uaminifu - timiza ahadi.
6. Usikate tamaa, na uhakikishe unapata kile ulichokusudia.
7. Jiwekee malengo,yaandike na uyatekeleze.
8. Heshimu mda wako, utumie mda vizuri kwa kufanya mambo ya muhimu.
KUNA BAADHI YA TABIA ZA KUACHA ILI UWEZE KUFANIKIWA KATIKA
JAMBO ULILOLIPANGA, AMBAZO NI ;
JAMBO ULILOLIPANGA, AMBAZO NI ;
{a}: Usidharau ulivyonavyo hata kama ni vidogo,kwani hakuna kitu kinachoanza na kikubwa, kama una kipaji,mitandao,ujuzi,elimu,fedha vitumie kwa ufasaha viweze kukuletea kitu kikubwa kwa baadae.
{b}: Usikae bila shughuli yoyote, kama hujapata kazi buni chochote kitakachokuongezea uthamani wako,uchukie uvivu na uchukie kukaa bila kazi.
{c}: Acha visingizio, kwani mafanikio ya mtu humtegemea yeye kwa zaidi ya asilimia 95.
{d}: Usiwe tegemezi wa mawazo,usiishi kwa mazoea,mkumbo au kufuata wanachotaka wengine, fanya unachoamini ni sawa.
{e}: Unapokutana na magumu au kuanguka,usikate tamaa,zingatia elimu uliyojifunza kupitia hayo magumu na uendelee mbele.
UBUNIFU KATIKA JAMBO LOLOTE KAMA
BISHARA NA MAISHA KIUJUMLA.
UBUNIFU: Ni kile kitendo cha kutekeleza wazo jipya ili kutatua tatizo,kutengeneza ama kuboresha bidhaa,huduma au kuongeza tija.
BISHARA NA MAISHA KIUJUMLA.
UBUNIFU: Ni kile kitendo cha kutekeleza wazo jipya ili kutatua tatizo,kutengeneza ama kuboresha bidhaa,huduma au kuongeza tija.
Umuhimu wa ubunifu.
- Unasaidia kuongeza na kupanuka kwa faida na katika biashara huongeza vivutio vya wateja.
- Unasaidia kuongeza na kupanuka kwa faida na katika biashara huongeza vivutio vya wateja.
- Ubunifu unaweza kurahisisha usimamizi wa biashara yako kwa kubana mianya yoyote yenye uzembe na wizi.
- Bila ubunifu biashara inaweza kuachwa nyuma na washindani kisha kufilisika.
Namna ya kujenga au kuleta ubunifu katika jambo au biashara.
- Kila wakati jiulize je?, kuna njia bora zaidi ya kufanya jambo unalolifanya?, hata baada ya kuboresha mara 100%, bado kuna fursa za kuboresha.
- Kila wakati jiulize je?, kuna njia bora zaidi ya kufanya jambo unalolifanya?, hata baada ya kuboresha mara 100%, bado kuna fursa za kuboresha.
- Usiwe mtumwa wa desturi na mawazo yaliyopo, kila mda jiulize bado zinatumika,zinahitajika au zinafaa?.
-Jaribu kufanya vitu vipya au vilevile kwa njia tofauti kila wakati.
tia comments and suggestions
ReplyDelete